UPENDO WISDOM K – Mungu wa Nyakati Zote Lyrics ( God of all Times)
UPENDO WISDOM K Mungu wa Nyakati zote Lyrics ( God of all Times)
Mungu wa nyakati zote, nakuabudu
Mungu wa wote wenye mwili, nakuabudu
Mwenye mamlaka yote, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote
Mungu unayeishi, nakuabudu
Mungu unayejibu, nakuabudu
Mzee wa siku, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote
Milimani mabondeni, gizani nuruni
Kiangazi au masika Kwenye raha au majonzi
Mkono wako waokoa, roho wako wafariji
We ni Mungu wa nyakati zote
Haulinganishwi na chochote
Hautetemeshwi na majira
Ulikuwako sasa uko na milele
Na milele utadumu
Alpha Omega mwanzo mwisho
Watangaza mwisho kabla ya mwanzo
Wewe ni Mungu wa nyakati zote
Ee Mungu mwenyezi, nakuabudu
Mungu mwenye enzi, nakuabudu
Mshika maagano, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu
Mungu mtukufu, nakuabudu
Mungu mtakatifu, nakuabudu
Mungu mkamilifu, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wewe ni Mungu wa nyakati zote
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Uweza wako ni wa ajabu
Yesu uweza wako ni wa ajabu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote