Mbosso Tamba Magufuli Lyrics

Nguru usimtoe chumvi
ndio ladha yake
Muunge tu nipe na chuzi
Na nyama yake
Eeh kula ya mbuzi
Ni kamba yake
Ye king’ amuzi ni dishi lake

 

Fungeni maturubai
(Mkeshe mkisema)
Wala hamtupi shida
(Mkeshe mkisema)
Ndo kwanza tunajidai
(Mkeshe mkisema)
Kama afisa wa nida oooh

 

Tena daktari nimekuja
na tiba sindano
(Leta nichomeke)
Chunga kibinda mwali
napita kwenye mabano
(Leta nichomeke)

Tena ngangari hodari wa mapambano
Acha wateseke
Na tupo na wewe baba mpaka mbili ishirini na tano
Acha wateseke

Tamba tamba, tumekupa uwanja tamba
Tamba tamba, warushe warushike roho zao
Tamba tamba, wenye majipu watumbue leo
Tamba tamba, tamba baba lao

Check Out:  Daddy1 - Main Danger Lyrics

Twaomba akulinde Mungu dua zetu sie
Fly over kama kwa wazungu
Tuna ndege zetu sio
Na hujatugawa mafungu yule na mie
Taifa moja sote kama ndugu
Ah chakula tukupatie

Umepambana na Tsunami
La korona ilipoingia, ni amani kote sasa
Rushwa na unyang’anyi
Tinga tinga umefagia mafisadi wote msasa

Hili ndo chama langu nimezama mazima, CCM!
Dando jiji langu makonda nalidima, CCM!
Makamu wa rais wangu mama Samia halima, CCM!
Majaliwa waziri wangu kata kata mashina , CCM!

 

Fungeni maturubai, mkeshe mkisema
Wala hamtupi shida, mkeshe mkisema
CCM twajidai, mkeshe mkisema
Kwetu ushindi kawaida ooh

Tena Magufuli amekuja na tiba sindano
Acha wateseke
Anachapa kazi babu ye hana mfano
Acha wateseke

Check Out:  Demarco - Kingston 20 Lyrics

Tena ngangari hodari wa mapambano
Acha wateseke
Na tupo na wewe baba mpaka mbili ishirini na tano
Acha wateseke

 

Tamba tamba, tumekupa uwanja tamba
Tamba tamba, warushe warushike roho zao
Tamba tamba, wenye majipu watumbue leo
Tamba tamba, tamba baba lao

Tushalinoa panga porini kukata muwa
Yaani tumejipanga wapinzani mtajijua
Tushalinoa panga porini kukata muwa
Yaani tumejipanga wapinzani mtajijua

Tushalinoa panga porini kukata muwa
Yaani tumejipanga wapinzani mtajijua
Tushalinoa panga porini kukata muwa
Yaani tumejipanga wapinzani mtajijua

Lalalala…. (Ayolizer)

Afrika Lyrics