Nacha – Barua Lyrics
Nacha Barua Lyrics
Nyasubi ndani ya mbanyu
Kiri, wamemchokoza Bea
Kwako ndugu hii ni barua ya wazi
Barua yenye mambo kadhaa sio ya kuomba kazi
Salamu habari za mda huu
Husika ana kichwa cha habari hapo juu
Mi nilifunzwa kusimama pale napokwenda chini
Nilifunzwa kuacha kazi pindi pale anapoadhini
Huu uandishi zaidi ya Ngug’i wa Thiong’o
Share Bandra bahati ya uandishi wa Sigongo
Nami nasikia sina uhakika kuhusu uzembe
Jibu kubakia simba alafu kuikataa mazembe
Vilabu ni taasisi nembo zalisha pesa
Ubaya wa kumtegemea mwarabu akinuna anaposti Twitter
Waliloweka miguu wasisinzie wakariri sana
Michoro ya test-tube na bunsen burner
Elimu ni kupanua akili mawazo chanya
Wanachofeli ni kutegemea kusoma waje kufanya
Kila kitu ni fursa hii nchi ina vituko
Mwenye mvi alitemwa huko leo kapokewa hukoo
Kumkumbatia anayekufilisi
Ni sawa na kuozesha mgumba kwa kasisi
Na hii barua sio kitabu cha Wayahudi
Torati ya Musa au Zaburi ya Daudi
Msilie masista duu wabishi mliokataa umama ntilie
Leo una mpa heshima Shishi
Kamri hii si ni dhawabu, mnajidanganya sasa
Pesa ya kamari kuchangia ujenzi wa madarasa
Barua hii bado ina kurasa nyingi
Endelea kusoma ndani utajifunza vingi
Ah-ah naomba msiniite mi nabii
Ambaye nimeshushwa kwa ukoo wa kizazi hii
Ah-ah mi nimeandika tu barua
Na sina maana kama nafaa kuitwa Masia
Chonde naomba msiniite mi nabii
Sikuwa na lengo baya kuandika barua hii
La hasha sitaki kutukuzwa
Mwenye akili atasoma na mpuuzi atapuuza
Na bongo kazi kubwa ni ile ya kutafuta kazi…