Roma – Diaspora Lyrics
Diaspora Lyrics by Roma
Tongwe Records Beiby
(Bin Laden)
Umwambie sikupenda, kuikimbia nchi yangu Kabla kalenda nimeondoka kabla ya mwanangu Na sijui ninapokwenda na simjui na mrithi wangu Usije ukambemenda mwanangu oii
Kitovu chake ukizike nilipopitisha unyayo Akiwa wa kike ndo furaha nitakayo Ukinizalia dume Inshallah ni hayo Nitampa jina la mtume na nitamuita Matayo
Akikuwa mwambie babake alikuwa mwanaharakati Na ukamwonyesha ununio ndio kumbukumbu iliyobaki Awaheshimu nduguze ambao walimwachia ziwa Wamdhamini wamtunze abadani asijione mkiwa
Na asinichukie mimi maana sikumchukia babu yake Akikuwa atajua kwanini na ataheshimu maamuzi yake Na uchunge ulimi aishike dini yamkini ana jini mkongwe Na umsikizishe yangu mapini —
Na ukipata usimsahau mama, mkumbuke na bibi Niombee nitusue mnyama, nabeba kavu msumbiji
Sijui nitakuona nitakufa sijui nitarudi Akikuwa mwambie Roma ndo baba we ndo shahidi
Uvumilie, utulie, umlilie Haya maisha ni safari Usilie,
uvumilie, umtulie na ulilie Haya maisha ni safari
Nafahamu utazaa kwa uchungu
Leba utalia na mengi yakidondoka chini ya uvungu
Atambeba malaika wengi
Mimba huja na kisirani, na kuna unavyotamani Kumvukuta sivo mfodhani ila siwezi rudia njiani
Na unafahamu hunnie ile nyumba uridhi haina vigae
So unaweza pima mzani ni budi ama nikomae Bora nikomae tu tujichange tumjengee mama kibanda Inshallah mpaka uzae nitakuwa nimejipanga
Na nimetuma picha yangu waonyeshe wanangu wasinisahau
Waambie baba atarudi uwape moyo angalau
Kuna muda nina hamu ya ngono ila sina hamu ya mapenzi
So please ongeza visomo kwa yule Ustadh wa Mbezi
Najua unanimiss ila jitunze nami nitakutunzia fimbo Walinde wanangu wao ndo warithi na ndizo za Roma simbo Wananiambia mashabiki Roma rudi uchukue jimbo Huku ukizingua polisi tu unawekewa goti la shingo
Basi ni hayo tu maisha ni mapambano ila sio sinza Na
usisahau kuwapa tano Dajide, Mada na Siza
Na uwaambie huku watu hawachagui kazi Ila majungu na umbea yaani vitu ni vingi mzazi
Uvumilie, utulie, umlilie Haya maisha ni safari Usilie, uvumilie, umtulie na ulilie Haya maisha ni safari
Uvumilie, utulie, umlilie Haya maisha ni safari
Tongwe Records Beiby (Bin Laden)