Mbosso – Karibu Lyrics Ft. Diamond Platnumz
Karibu Lyrics by Mbosso Ft. Diamond Platnumz
Ishafika saba sasa, tunakungojea
Imebaki miezi miwili tu, ebu siku sogea
Tuna shauku na bashasha, ya kukupokea
Sio mimi na mama yako tu, na bibi anakuombea
mmmmmmh….
Imani yangu inanituma, unanisikia baba yoo (baba yo yo)
Na furaha yangu dongo kumung’unya, anapobugia mama yoo (mama yo yo)
Mmh, gari li wazi wazi, kuwa muda usha tawakal
Natamani useme zawadi ila acha ninunue vigari
Oooh kuna shangazi kibiti kwa mzee kikali
Ukiota meno wataleta viazi ule mihogo uwe ngangali
Ule mihogo uwe ngangali
Kwanza nitakupa jina gani (tarara tarara raraara tarara)
Kwanza karibu duniani baba (tarara tarara raraara tarara)
Kwetu furaha isiyo kifani (tarara tarara raraara tarara)
ila kuna mengi duniani baba (tarara tarara raraara tarara)
Mmh, kwa furaha niliyonayo, ngechinja ng’ombe kwa tambiko
Ila baba yako uwezo sina, pokea uji kwa kijiko
Pokea mwanangu (ai yo yo)
Tena awape habari, waropokaji wapambe
We ni wangu wa halali, wasije zani vya nyange
Dunia ni mafuriko vua koti,
Wanadamu mioyo ya matope
Ukitukanwa, mwiko usiogope
Jikawe mwana wa Dangote
Ooh, wasimuone
Kimasomaso wasimuone
Wenye jicho la chuki wasimuone mwanangu
Kimasomaso wasimuone
Ooh, wasimuone
Kimasomaso wasimuone
Wenye jicho la chuki wasimuone mwanangu
Kimasomaso wasimuone