Zuchu – Wana Lyrics
Zuchu Wana Lyrics
(Ayolizer)
Unywe maji ya kapita
Mi ni kiguu na ushafika
Jina gani hujaniita beiby
Ujeuri hutaki kabisa
Eti unachenga visa
Vya Firauni vya Musa vingi
Nikilala naota kama unaniita
Nafumba macho, navuta shuka
Naona napumbazika
Unishikapo ndipo hapo
Nafarijika
Mambo yako, mahaba yako
Ndo maana natononoka wee
Wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana
Nzi kidondani ufio
Wahenga walisema
Maradhi yaweza yasiwe na dawa
Kwa penzi yakapona
Rabii, amenipa nusura
Jeuri sina tena
We ndo ganzi, umenimaliza hasira
Siungi wakisema
Nidekeze, niliwaze
Washushuke wanyamaze
Mi kidonda nibembeleze
Usinipepee nipulize
Watume wash!tuke
Roho zao ziwaume
Mi nipike ule chote
Unenepe upendeze
Wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda univimbe nikumbatie
Ata watu watuone wakahadithie
Nitambulishe niringe niwavimbie
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda univimbe nikumbatie
Ata Laizer atuone wakahadithie
Nitambulishe nitambe niwavimbie
(Wasafi)