Harmonize – Tuvushe Lyrics
Tuvushe Lyrics by Harmonize
Taifa limeishapata suluhu
Kinachofata ni mipango na
Majaliwa ya mwenyezi Mungu
Analilipanga Mungu huwezi kulipangua
Alitupa Magufuli kisha akamchukua
Amekuachia jaahazi na sisi ndio abiria
Jukumu letu ni kuchapa kazi
Maana yupo wa kusimamia
Tutumbulie majambazi wala rushwa na maharamia
wasiotaka kufanya kazi wapenda pesa za kuvizia
Mama tuvushe
Taifa zima lina imani na wewe (tuvushe)
Hayati JPM alikuteuwa wewe (Mama Samia tuvushe)
Taifa zima tunakutazama wewee
Mamaa (tuvushe)
Eeh Refarii ndio kabadilika
Lakini uwanja ni ulele
Kazi juu ya kazi
Tena mpenda haki mtu wa Mungu
Fitna hataki wala majungu
Eee na ndoto za wanawake shupavu zimetipia
Na huyu ndio rais wa kwanza mwanamke hapa Tanzania
Mama Samia, anakwenda kumalizia
Miradi iyobakia
Pole yenu mnaoofia
Aa Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Usisi, Bigi na serenda madaraja yote
Aa Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Na fly-over zilizobakiaa
Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Standard gauge, air Tanzania
Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Mabarabara, Elimu bure pia
Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Mradi wa umeme bwawa la nyerere
Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza
Ikulu chamwino Dodoma izidi songa mbele
Mamaa Waonyeshe Unavyotekeleza